MADEE NA VIDEO YA STORI YAKE


MSANII wa muziki wa kizazi kipya toka kundi la Tip Top Connection,  Ahmed Ally ‘Madee’ ameanza kurekodi video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Stori’.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Madee alisema kuwa kazi ya kurekodi video hiyo inafanywa na Adam Juma ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Visual Lab.
Alisema pamoja na kuanza kuufanyia video wimbo huo katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam bado hajauachia katika vituo vya redio na  atafanya hivyo hivi karibuni.

Comments