Skip to main content

MABADILIKO MISS WORLD YAATHIRI MISS TANZANIA





Mkurugenzi wa Lino International Agency inayoratibu shindano la Miss tanzania Hashim Lundenga akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na mabadiliko ya mashindano hayo, kushoto ni mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania Albert Makoye na kulia ni Mshauri wa kamati hiyo, Dk.Ramesh Shah
PRESS RELEASE
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

15  MACHI 2012

MABADILIKO YA KALENDA YA  MASHINDANO YA UREMBO YA DUNIA:


Katika mkutano wa mawakala wa wanaoandaa mashindano ya urembo kutoka nchi mbalimbali duniani uliofanyika London Uingereza mwezi Novemba 2011, Tulijulishwa mabadiliko ya Kalenda ya mashindano ya urembo ya dunia.  [Miss World.]

Mashindano ya urembo ya Dunia yanatarajia kufanyika mwezi August 2012 nchini China, badala ya mwezi Novemba/ Desemba kama ilivyozoeleka, ambapo washiriki kutoka nchi mbalimbali watatakiwa wawe wamefika  nchini China mwezi Julai 2012.

Kutokana na hali hiyo tunalazimika kubadilisha kalenda ya mashindano yetu kama ifuatavyo:-

1. Tutatuma Mwakilishi atakayeshiriki mashindano ya urembo ya Dunia Miss World 2012.

2. Mwakilishi  huyo atapatikana kwa njia ya usaili.  Ambapo warembo watakaojitokeza
    katika usaili huo  watafanyiwa  mchujo na kupatikana   idadi ya warembo 10  watakao
    panda jukwaani katika tafrija ndogo ili kumpata Mwakilishi  ambaye atabeba Bendera ya
   Tanzania katika Fainali za Mashindano ya urembo ya Dunia   2012.

3. Tunaomba warembo wote wenye sifa na nia ya kushiriki  katika mchujo wa usaili
    wawasiliane na ofisi zetu au Mawakala wete popote Tanzania kupata maelezo zaidi.

 Mchakato wa mashindano ya Redds Miss Tanzania 2012 katika ngazi zote utaendelea kama kawaida  na Mshindi wa Redds Miss Tanzania 2012 atawakilisha nchi yetu katika Fainali za Mashindano ya urembo ya Dunia mwaka 2013, akiwa na muda wa miezi [7] saba ya maandalizi.

Hii inakidhi haja na maoni ya Wadau wa fani ya urembo ya kumpa muda wa kutosha Mrembo wa Taifa kujiandaa vya kutosha kabla ya kushiriki Fainali za dunia.

Lundenga
HASHIM LUNDENGA.
MKURUGENZI.



Comments