LIVERPOOL YAPATA BONGE LA PIGO


BEKI wa Liverpool, Daniel Agger atakuwa nje ya Uwanja kwa wiki kadhaa, baada ya kuumia mbavu katika fainali ya Carling Cup timu yake ikishinda dhidi ya Cardiff City, kocha wake Kenny Dalglish amesema jana.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Denmark, ambaye amekuwa akitubuliwa na majeruhi mara kwa mara, alitolewa nje dakika ya 86 Jumapili, timu yake ikishinda kwa penalti na sasa anatarajiwa kuikosa mechi ya Jumamosi dhidi ya Arsenal katika Ligi Kuu.
"Amechanika mbavu, hivyo atakuwa nje kwa wiki chache," alisema Dalglish katika tovuti ya klabu hiyo,  (www.liverpoolfc.tv).
"Mtu yeyote anayeumia anaacha pengo. Daniel amekuwa akicheza vizuri sana mwaka huu, lakini tutamkosa mtu yeyote ambaye hayuko fiti  na yupo.
"Kikosi kipo kwa ajili ya kuziba mapengo, walio majeruhi na waliosimamishwa, kwa Daniel kama atakuwa nje kwa wiki kadhaa."
Liverpool pia itamkosa Nahodha wakle Steven Gerrard katika mchezo wa Jumamosi baada ya kutolewa nje kwenye mechi ya kirafiki ya timu yakie ya taifa, England ikifungwa na Uholanzi Jumatano kutokana na kuumia nyama za paja.
"Kama sifahamu anaendeleaje, siwezi kukuambia kama kuna nafasi yoyote au hakuna (kwa Gerrard kuivaa Arsenal)," alisema Dalglish.
"Hivyo kuliko kubashiri, ni vizuri kwetu kusubiri na kuona nini madaktari watasema baada ya kumfanyia uchunguzi."

Comments