Viingilio kwenye mechi namba 149 ya Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) kati ya Moro United na African Lyon itakayochezwa kesho (Machi 24 mwaka
huu) Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam
ni sh. 1,000 kwa mzunguko na sh. 5,000 kwa jukwaa kuu.
Mwamuzi Hashim Abdallah wa Dar es Salaam ndiye atakayechezesha mechi
hiyo akisaidiwa na Ephraim Ndissa na Abdallah Selega wakati mwamuzi wa akiba ni
Oden Mbaga. Wote pia wanatoka Dar es
Salaam . Kamishna wa mechi hiyo ni James Mhagama kutoka
mkoani Ruvuma .
Pia viingilio hivyo ndivyo vinavyotumika kwa mechi zote za
Ligi Kuu ya Vodacom zinazochezwa Uwanja wa Chamazi zisizohusisha timu za Simba
na Yanga.
VPL itaendelea tena Machi 28 mwaka huu kwa mechi kati ya
Ruvu Shooting Stars itakayocheza na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini
mjini Mlandizi wakati Moro United itakuwa mwenyeji wa Villa Squad katika mechi
namba 153 itakayofanyika Uwanja wa Chamazi.
Comments
Post a Comment