KUWAONA SIMBA,ES SETIF BUKU 5


Viingilio katika pambano la Jumapili ijayo kati ya Simba na ES Setif vitakuwa ni Sh 5,000 kwa viti vya kijani na bluu. Sh 10,000 viti vya rangi ya chungwa. Sh 15,000 VIP C, Sh 20,000 VIP B na Sh 25,000 VIP A.
Tiketi zitaanza kuuzwa Ijumaa ijayo katika vituo vifuatavyo. Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Big Bon Kariakoo, Zizou Fashion Sinza na Kijitonyama, Robby One Fashion Kinondoni Studio, Uwanja wa Taifa, Dar Live Mbagala Zakheem na Gongo la Mboto kwenye Duka la Michael Maluwe.
Usalama utazingatiwa sana. Kutakuwapo na kamera maalumu za kutambua wavunjifu wa amani na waharibifu wa uwanja na wananchi wanaombwa kutojihusisha na vitendo vya aina yoyote vyenye kuvuruga amani.

SIMBA NA SETIF

TIMU ya Setif imeingia nchini leo alfajiri na ikiwa na msafara wa watu 35 wakiwamo wachezaji 20, benchi la ufundi, viongozi wa Shirikisho la Soka la Algeria na waandishi wa habari.
SIMBA imeingia kambini Dar es Salaam jana na serikali imetoa ruksa kwa Wekundu wa Msimbazi kufanya mazoezi katika Uwanja wa Taifa katika siku zilizobaki kabla ya mechi ya Setif.
Hata hivyo, mazoezi hayo hayaruhusiwi kuhudhuriwa na washabiki na hivyo uongozi wa Simba unaomba washabiki wasije uwanjani kuangalia mazoezi.
Tukutane kwenye mechi Jumapili.
Ezekiel Kamwaga
Simba SC

Comments