KOCHA WA ZAMANI CHELSEA AWAONYA MAKOCHA WASIBABAKIE OFA ZA ABRAMOVICH


KOCHA wa zamani wa Chelsea, Luiz Felipe Scolari amesema kufanya kazi chini ya mmiliki wa klabu hiyo, Mrusi Roman Abramovich ni sawa na kuingia ‘jehanam’.
Luiz Filipe Scolari ameonya atakayetaka kurithi mikoba ya Villas-Boas aliyetimuliwa Jumapili, ajue hilo.
Abramovich kwa sasa anamtafuta kocha wa nane wa kudumu tangu mwaka 2003 baada ya kumtimua Andre Villas-Boas siku ya Jumapili.
"Itakuwa sawa na kuingia kuzimu kwa yeyote atakayechukua nafasi ya Villas-Boast," alisema Scolari,ambaye aliwahi kuwa meneja wa Chelsea kwa miezi saba kati ya mwaka 2008-09.
"Kumtimua lilikuwa jambo la ajabu, ingawa si ajabu sana kwangu kwa sababu ya kile nilichokumbana nacho nilipokuwa katika klabu ile.

Comments