FERGUSON ASEMA BINGWA ENGLAND ATAJULIKANA APRIL


KOCHA Sir Alex Ferguson anaamini bingwa wa Ligi Kuu England ataamuliwa kwa mpambano wa wapinzani wa jadi katika Jiji la  Manchester, Man United watakaposafiri kuwafuata vinara wa sasa wa ligi hiyo, Manchester City kwenye Uwanja wa Eastlands, Aprili 30, mwaka huu.
Kocha wa United, Ferguson anashawishika kwamba timu yake imepiga hatua kubwa katika mbio za kutetea taji lakekufuatia ushindi wa 3-1 dhidi ya Tottenham Jumapili.
Mabingwa hao waliwekwa katika wakati mgumu kwenye mchezo huo, lakini wakanufaika na makosa ya walinzi wa Spurs, yaliyotumiwa vizuri na Ashley Young aliyepachika mabao mawili kwenye mechi hiyo.
Ferguson anakubali kwamba timu yake ina bahati, lakini anaamini kiwango cha juu kinachoonyeshwa na United tangu kuanza kwa mwaka huu kinawatia presha City, ambao kwa sasa wanaongoza ligi hiyo kwa pointi mbili zaidi.
"Tumekutana na timu zote kubbwa tangu Januari ikiwemo City na Liverpool kwenye Kombe la FA Cup," alisema Ferguson.
"Tumepita kote huko na wachezaji wamefanya vizuri. Wamecheza vizuri kwenye mechi nyingi,"aliongeza. 
United itaivaa City mwishoni mwa Aprili katika mechi ya tatu kuelekea mwisho wa msimu na Ferguson alisema: "Nafikiri itakuwa (ya kuamua bingwa), ndio,".

Comments