KIYOVU YAMUWEKA NJE YA DIMBA MWINYI KAZIMOTO


WAKATI kesho itashuka kwenye dimba la Taifa Dar es Salaam kucheza mechi ya ligi kuu bara dhidi ya Kagera Sugar ya Kagera, Wekundu wa Msimbazi Simba watamkoa mshambuliaji wake Mwinyi Kazimoto ambaye alichanika nyama za paja katika mchezo wa kombe la Shirikisho (CAF) baina ya Simba na Kiyovu jumapili.
Kutokana na maumivu hayo, itamlazimu Kazimoto  kuwa nje ya dimba kwa siku kumi,  hivyo kuungana na majeruhi wengine Juma Jabu na Ulimboka Mwakingwe.

Comments