KIYOVU YA RWANDA YAPIGWA 2-1 NA SIMBA YA TANZANIA

Mchezaji wa timu ya Simba mganda Emmanuel Okwi kulia akijaribi kumtoka mchezaji wa timu ya Kiyovu ya Rwanda wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho katika ya timu hiyo na Kiyovu ya Rwanda unaofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii. 
 
 
 
Simba imefanikiwa kuiondosha Kiyovu ya Rwanda magoli 2-1, magoli ya Simba yamepatikana katika kipindi cha kwanza na yamefungwa na mshambuliaji Felix Sunzu akipokea pasi nzuri, kazi iliyofanywa na mchezaji Emmanuel Okwi wa Simba. Timu ya Kiyovu imepata goli lake la kufutia machozi  katika kipindi cha pili cha mchezo huo, kwa matokeo hayo,  Simba imefanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho barani Afrika,

 Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia vilivyo wakati timu yao ilipokuwa ikichuana na timu ya Kiyovu ya Rwanda katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barabi Afrika uliofanyika leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.



Comments