KIVUMBI LIGI YA MABINGWA ULAYA


MABINGWA wa zamani Inter Milan na Bayern Munich leo watashuka dimbani wakiwa na presha kubwa ya kuraka kutimiza ndoto zao za kufuzu kwa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Inter watakuwa wenyeji wa Olympique Marseille, huku Bayern Munich watawakaribisha Basel wakati dunia ikisubili kuona miujiza mingine.
Kocha wa Inter Milan, Claudio Ranieri anaamini atalia kwa aibu kama timu yake itashindwa kufuzu kwa leo.
Inter iliyoshinda mechi ya kwanza kati ya 10 ilizocheza kwenye mashindano yote ilipoichapa Chievo Verona 2-0  katika Serie A siku ya Ijumaa na kusababisha kocha wao Ranieri kutokwa na machozi.
Mabingwa hao wa 2010, Inter wataingia uwanjani wakiwa nyuma kwa bao 1-0 waliofungwa na Marseille wakifanya uzembe wowote leo wataaga michuano hiyo.
ìKuwa na hisia ni kitu kizuri. Nafanya kazi hii kwa hisia zangu zote hasi na chanya, lakini ukweli ni kwamba chanya ndio bora,î alisema.
ìNatumaini mechi yetu ya leo dhidi ya Marseille kwenye Uwanja wa San Siro itakuwa na mashabiki wengi wa kutushangilia. Haitokuwa mechi rahisi, lakini tutajaribu kupata matokeo mazuri.î
Ndoto ya Bayern Munich kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa kwenye uwanja wao ipo shakani leo kama watashindwa kusawazisha kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa FC Basel.
Pamoja na kuichakaza Hoffenheim 7-1 katika Bundesliga pale Jumamosi, Bayern wanaonekana wanahofu dhidi ya Basel yenye lengo la kuwa timu ya kwanza ya Uswisi kufuzu kwa nane bora ya michuano hiyo baada ya kupitia miaka 33.
ìUshindi wetu dhidi ya Hoffenheim umetupa kujiami kwa ajili ya mechi ya leo,î alisema kocha Jupp Heynckes.
Bayern, uwanja wake utakuwa mwenyeji wa fainali ya mwaka huu, hapo imeshinda mechi 11 kati ya 12 ilizocheza Uwanja wa Allianz Arena.

Comments

  1. Ahsante ndugu yangu kwa kutujali tusio ma macho maangavu....Tupo pamoja

    ReplyDelete

Post a Comment