KINDA LA YANGA LACHOKOZA MAUMIVU


HUKU akidhani amepona kabisa maumivu ya enka, mchezaji chipukizi wa klabu ya soka ya Yanga Salum Telela juzi alijikuta akiugulia maumivu baada ya kujaribu kuanza kufanya mazoezi.

Telela amesema kuwa baada ya kuumia kwa wiki kadhaa alikuwa akijitibia kabla ya kuona hali yake imetengermaa na kuanza mazoezi lakini matokeo yake amejikitu kama anatonesha kidonda.

"Kweli nilikuwa na maumivu ya enka yaliyoniweka nje ya dimba kwa wiki kadhaa baada ya kujitibu nilipata ruhusa na daktari wangu kuanza mazoezi mepesi lakini nilipojaribu nilipata maumivu makali,"Alisema.

Kutokana na hali hiyo, Telela alisema atalazimika kuendelea kujitibuy mpaka hali itakapotengemaa kwanza.

Comments