KANYE WEST ABUNI VIATU VYA KINADADA


NEW YORK, Marekani
RAPA Kanye West amebuni viatu vyake vya kike ambavyo ataviuza kwa akina dada kwa kupitia Kampuni yake ya Dw kwa kushirikiana na Collete ya Ufaransa ambayo imeshiriki katika maonesho yaliyopewa jina la Paris Fashion Week mwaka 2012.
Viatu hivyo vya rapa huyo vinatarajiwa kuuzwa kati ya dola 6,000 au euro 4,420 kwa mujibu wa kampuni inayoletea kutoka Ufaransa.
Viatu vyake hivyo vinamng’aro ulionakshiwa kwa madini mbalimbali, vikiwa vinapatikana katika maduka makubwa ya Harper Bazaar Australia na Italia ambako ndiko kumebuniwa na mbunifu wa nchini humo, Giuseppe Zanotti.
Rapa huyo ambaye kwa sasa anajihusisha na masuala ya uajasiriamali wa urembo alionesha kuvutiwa na mtindo ya onesho hilo la mwaka huu.

Comments