KAMPUNI LIGI KUU, KASHESHE LAIBUKA UPYA




MKAKATI wa uundwaji wa kampuni ya kusimamia Ligi Kuu ya Tanzania Bara umefufuliwa leo kwa kikao kilichofanyika kwenye hoteli ya JB Belmonte katikati ya Jiji ya Dar es Salaam.
Katika kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti Geoffrey Nyange 'Kaburu' na Katibu Celestine Mwesigwa, klabu 10 zilihudhuria na nne tu viongozi wake hawakuweza kufika ambazo ni Ruvu Shooting, JKT Oljoro, Kagera Sugar na Mtibwa Sugar.
Klabu zimefikia mwafaka wa kumuagiza mwakilishi wa Coastal Union ya Tanga, Wallace Karia ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati yua Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwsilisha hoja zao kwa Kamati ya Utendajiya TFF, ili suala lao lijadiliwe katika Mkutano Mkuu, utakaofanyika Machi 24, mwaka huu.
Ligi Kuu inaendeshwa na TFF, lakini klabu zinataka TPL ianze kuendesha ligi hiyo kuanzia msimu ujo na msimamo ulikuwa mkali katika kiko cha leo.
Klabu zitakutana tena Jumapili ili kumalizia mchakato wa hoja zitakazowasilishwa na Karia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi Kuu iliyoundwa na TFF kwenye Kamati ya Utendaji ya TFF.

Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHMarch 12, 2012 at 8:56 AM

    MBONA HAYASOMEKI,REKEBISHENI HALI HII INASABABISHA USUMBUFU NAONA KAMA MNAANZA KUIZOEA NA KUIONA YA KAWAIDA

    ReplyDelete

Post a Comment