KALAPINA:NIMEKUWA SASA,SIFANYI UJINGA

NYOTA wa muziki wa hiphop nchini Kalama Masoud 'Kalapina' amesema sasa amekuwa mtu mzima hivyo ameachana na mambo ya kijinga ambayo alikuwa akifanya siku za nyuma.
Kala ambaye pia ni mwanachama wa kundi la Kikosi cha Mizinga amesema kutokana na kuwa na familia hana sababu ya kufanya mambo ya ajabu ambayo yatamshushia heshima.
"Nina mke na mtoto mdogo hivyo itakuwa ni aibu kama mwanagu atakuwa akiona baba yake anafanya mambo ya hovyo...hata kuimba pia nimebadili aina ya uimbaji wangu na hasa katika ujumbe,"Alisema

Comments