ALEX KAJUMULO KUGOMBEA UONGOZI TFF

MDAU wa soka aliyepata kumiliki timu ya soka ya Sigara, Alex Kajumulo amesema anakusudia kuwania uongozi katika Shirikisho la sOKA tANZANIA (TFF).
Akizungumza katika kipindi cha michezo cha Redio Clouds, Kajumulo anayeishi nchini Marekani alisema kama Mtanzania anapaswa kuwania uongozi katika klabu hiyo na amepata msukumo huo baada ya kutoridhishwa na utendaji wa viongozi wa soka la Bongo.
"Nitajitosa kugombea moja ya nafasi katika uchaguzi ujao wa TFF....ila sitarajii kugombea urais, nafanya hivyo kwa lengo la kutaka kuiweka pazuri soka ya Tanzania kupitia mimi kuwa ndani ya uongozi,"Alisema Kajumulo.
Pamoja na michezo Kajumulo ambaye pia ni mfanyabiashara, amejitosa katika tasnia ya muziki akiimba mtondo wa Regge.

Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHMarch 10, 2012 at 7:45 AM

    ALEX NJAA ANAIWEZA HUYU MTU,NIMEKUBALI...KUNA SIKU NILIINGIA KWENYE ACCOUNT YAKE YA TWITTER ANAJITAMBULISHA KAMA MTETEZI WA MASHOGA AFRICA!MWENYEWE NILIKOMA...!

    ReplyDelete

Post a Comment