JUVE YAUA 5-0


KIBIBI kizee cha Turin, Juventus jana kilizima gundu la kucheza mechi nne bila ya kushinda, baada ya kuirarua 5-0 Fiorentina, ambayo ilicheza zaidi ya saa moja na wachezaji 10.
Ikiwa bado haijafungwa msimu huu, Juve iko nafasi ya pili ikiwa inazidiwa pointi nne na vinara AC Milan baada ya vinara hao kushinda 2-0 dhidi ya Parma, mabao  ya Zlatan Ibrahimovic kwa penalti na Urby Emanuelson.
Milan, ambayo ilimuingiza uwanjani Gennaro Gattuso mwishoni mwa mchezo kwa mara ya kwanza tangu apate matatizo ya macho  Septemba, mwaka jana sasa ina pointi 60 kutokana na mechi 28.
Mabao ya Jube yalifungwa na Mirko Vucinic dakika ya 5, Chilean Arturo Vidal kabla ya mapumziko, Claudio Marchisio, Andrea Pirlo Simone Padoin walifunga mabao mengine

Comments