JUMA JABU KUIVAA ES SETIF

BEKI wa Simba aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu Juma Jabu 'JJ' huenda akawa mmoja ya wachezaji wa timu hiyo watakaocheza mechi ya marudiano ya kombe la Shirikisho (CAF) dhidi ya Es Setif ya Algeria wiki ijayo.
JJ ambaye alikuwa anakabiliwa na maumivu ya kifundo cha mguu alianza mazoezi na wenzake juzi katika kambi ya timu hiyo iliyopo Bamba Beach Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Comments