HOMA YA KESHO DHIDI YA YANGA, WACHEZAJI COASTAL WANYANG'ANYWA SIMU

COASTAL UNION

Homa ya mechi ya ligi kuu soka Tanzania Bara baina ya Coastal Union ya Tanga dhidi ya Yanga zitakazokwaana kesho baada ya uongozi wa Coastal kuwanyang'anya simu wachezaji wake.
Habari kutoka Tanga zinaeleza kuwa uongozi umefikia hatua hiyo ili kukwepa hujuma yoyote wanayoweza kufanyiwa na wapinzani wao.
Mechi hiyo imetokea kuwa gumzo ambapo viongozi wa Coastal na wale wa Yanga wakionekana kurushiana vijembe vya hapa na pale, huku Coastal wakilalamika hatua ya kamati ya nidhamu na Usuluhishi ya TFF kuwaondolea kwa muda adhabu wachezaji wa Yanga ambao walikuwa kifungoni kutokana kumpiga mwamuzi Israel Nkongo walipokwaana na Azam hivi karinbuni.
Kama hiyo haitoshi kila timu imetamba kushinda mchezo huo.

Comments