ES SETIF WAMUHOFIA KASEJA

WAPINZANI wa Simba katika kombe la Shirikisho (CAF) Es Setif ya Algeria wamesema kuwa Simba inabebebwa zaidi na kipa wao Juma Kaseja.
Kocha wa Es Setif Hakim Sebaa amesema kwamba wanauhakika wakufanya vema katika mchezo wao wa kesho kwenye dimba la Taifa lakini kinachowauimza kichwa ni ubora wa Kaseja pale langoni.
"Nina kikosi imara na kilichotayari kuwafunza kazi Simba kwani ni timu ambayo tunaimudu katika nafasi za ndani lakini kazi itakuja lango kwani kipa wake yule (Kaseja) ni moto wa kuotea mbali,"Alisema.
Timu hizo leo zinafanya mazoezi katika uwanja wa taifa tayari kwa mchezo wao utakaorindima kuanzia saa 10 jioni.

Comments