ES SETIF KUTUA NCHINI KESHO


WAKATI kikosi cha timu ya soka ya Simba kinatarajiwa kuingia kambini
leo kujiandaa na mechi yake ya kombe la Shirikisho 
dhidi ya ES Setifya Algeria, wapinzani wao hao wanatarajiwa kuwasili nchini kesho tayari kwea mchezo huo wa kwanza  utakaopigwa jumapili katika dimba laTaifa jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage alisema msafara wa watu 37 kutoka Algeria utafikia katikahoteli ya Durban iliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Alisema maandalizi kwa ajili ya mchezo huo yanakwenda vema ambapo kikosi cha Simba kilichopewa mapumziko ya siku moja baada ya kutoka Morogoro ilipocheza na Mtibwa Sugar ya huko na kuchanua na ushindi wamabao 2-1, kitaingia kambini katika hoteli ya Bamba Beach iliyopo Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Rage aliongeza kuwa kikosi chake kipo katika hali nzuri na kwa sikuzilizosalia kabla ya mchezo huo anaamini kocha mkuu wa timu hiyo Mserbia Milovan Cirkovic atazitumia vema kukiweka katika hali nzurizaidi ili kuweza kushinda mechi hiyo.

Mechi hiyo itakayopigwa kuanzia saa 10 kamili jioni itachezeshwa na waamuzi kutoka Rwanda ambapo mwamuzi wa kati atakuwa Hudu Munyemana wakati wasaidizi wake ni Felicien Kabanda, Theogene Ndagijimana na
Edouard Bahizi. Kamishna wa mechi hiyo ni Felix Tangawarima kutoka Zimbabwe.

Timu hizo zitarejeana Algeria Aprili 6  na iwapo Simba itashindaitacheza mechi ya kwanza nyumbani Aprili 29 mwaka huu na mshindi kati ya El Ahly Shandy ya Sudan na Ferroviario de Maputo ya Msumbiji ambapoya marudiano itachezwa kati ya Mei 11, 12 na 13 mwaka huu.


Comments