Dk.FENELLA KUZINDUA TIGO PESA YA TWIGA STARS


Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangala anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kuchangia timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) kupitia Tigo Pesa. 
Uzinduzi huo wa akaunti maalumu ya Twiga Stars kupitia mtandao wa Tigo utafanyika kesho (Machi 10 mwaka huu) saa 5 kamili asubuhi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Twiga Stars iko kwenye mashindano ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) ambapo Mei 26 mwaka huu itacheza na Ethiopia jijini Addis Ababa.
 

Comments