BOSI WA SOKA AJIUA KWA BAADA YA KIHORO CHA KASHFA YA KUPANGA MATOKEO

KLABU ya REAC ya Hungarian ambayo inakabiliwa na kashfa ya kupanga matokeo, imepata pigo baada ya Mkurugenzi wake, Robert Kutasi kudaiwa kujiua.
Taarifa ya timu hiyo yenye maskani yake Budapest, imesema leo kwamba Robert Kutasi alifariki Alhamisi. Taarifa ya Polisi ilisema alijiruisha kutoka ghorofani. Alikuwa ana umri wa miaka 48.
Wachezaji sita wa REAC walipelekwa Polisi Jumanne kwa kuhojiwa juu ya skendo ya kupanga matokeo, ambayo hadi sasa watu 25 wamekwishahojiwa.
Pamoja na wachezaji wa timu hiyo kufikishwa rupango, lakini viongozi wa REAC hawahusishwi katika skendo hiyo.
Kutasi aliyekuwa kinara wa mapambano dhidi ya rushwa katika soka ya Hungary, aliliambia gazeti la kila siku la Nemzeti Sport wiki hii kwamba; “Maisha yangu yameisha” kwa sababu ya kesi.

Comments