BMT YAMFUNGIA MAISHA KATIBU MKUU WA JUDO


Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu , Usuluhishi na Rufaa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Alex Mgongolwa (katikati) akitoa tamko leo jijini Dar es salaam la kumfungia maisha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Judo Tanzania Shaban Kashinde Bundala kutojihusisha na mchezo huo na mingine kwa kujihusisha na usafirishaji wa watu nje ya nchi kwa kisingizio cha kuwa wanamichezo bila kibali cha BMT. Wengine ni Msemaji wa BMT Maulid Kitenge (kulia) na Katibu Mkuu wa BMT Henry Lihaya(kushoto) 
Na Tiganya Vincent-MAELEZo-Dar es alaam

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limemfungia maisha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Judo Tanzania Shaban Kashinde Bundala kutojihusisha na mchezo huo na mingine kwa kujihusisha na usafirishaji wa watu nje ya nchi kwa kisingizio cha kuwa wanamichezo bila kibali cha BMT. 

Tamko hilo limetolewa leo jijini na Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu , Usuluhishi na Rufaa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Alex Mgongolwa (katikati) wakati akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) mjini Dar es salaam. 

Alisema kuwa Kamati hiyo imeridhika na yaliyobainika katika sakata hilo bila shaka yoyote kuwa Bundala amekuwa akijihusisha na usafirishaji wa watu nje ya nchi kwa kisingizio cha kuwa wanamichezo kwa kisingizio cha kwenda kushiriki mashindano yanayoandaliwa katika nchi mbalimbali bila kibali cha BMT. 

Mgongolwa amesema kuwa BMT imebaini kuwa Bundala alikuwa anajihusisha na mipango ya kusafirisha watu nje ya nchi kwa kisingizio kuwa ni wanamichezo wanaokwenda kushiriki katika michezo iliyoandaliwa huko bila ruksa wala kibali kutoka BMT huku akitambua ni kosa.

Alisema kwa mfano mwaka 2011 alisafirisha watu wapatao 27 akiwemo yeye mwenyewe mpaka Nairobi Kenya kwenda kuomba Viza za Ubalozi wa Poland ambapo baadhi yao walinyimwa Viza baada ya kuwasilisha nyaraka bandia na hivyo kusababisha Ubalozi kuwalisiana na Serikali juu ya uhalali wa shuguli za Bundala. 

Mgongolwa aliongeza kuwa mwezi Oktoba 2011 Bwana Bundala aliwasilisha majina ya watu 18 katika Ubalozi wa ufaransa kuomba Viza ya kuingia nchini humo hata hivyo baada ya kuchambuliwa ilibainika kuwa nyaraka za majina ya watu hao nyingi zao zilikuwa batili na BMT aikuwa na taarifa juu ya safari hiyo.

Aidha BMT inatoa tahadhari kwa vikundi na vyama vya michezo kuacha kutumia michezo kama njia ya kufanya amambo yao mengine amabyo siyo ya kimichezo kwa kutumia mgogo wa michezo. 
Alisema kuwa hali hiyo inachafua sura ya nchi na kurudisha nyuma maendeleo ya michezo nchini . 
Wakati huo huo Msemaji wa BMT Maulid Kitenge alisema kuwa Baraza hilo linatarajia kujadili na kutoa uamuzi juu ya mgogoro uliodumu kwa muda mrefu baina ya aliyekuwa Katibu wa CHANETA Anna Kibira na CHANETA.
 Alisema kuwa uamuzi huo utatolewa siku Jumamosi tarehe 10.03.2012 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Comments