BERKO AREJESHA MATUMAINI YANGA SC


HATIMAYE mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara, Yanga wamerejesha matumaini ya kushinda mechi zao baada ya kupona kwa kipa wake namba moja Mghana Yaw Berko.
Berko aliyekuwa nje ya dimba kwa siku kadhaa akikabiliwa na majeruhi ya mguu ameanza rami mazoezi leo asubuhi wakati timu hiyo ilipojinoa katika uwanja wa Kaunda jijini Dar es Salaam.
Yanga kwa sasa inaendelea na mazoezi yake ya kawaida kujiandaa na ligi hiyo ambapo Machi 31 itashuka katika dimba la Mkwakwani, Tanga kukwaana na Coastal Union ya huko.

Comments