Katibu
Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego (kulia) akionesha kitabu cha Sera ya Taifa
ya Utamaduni kwa viongozi na wamiliki wa Bendi za jijini Dar es Salaam kwenye
semina iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii. Kulia ni Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa,
BASATA Bi. Vivian Shalua.
Mkurugenzi
wa Bendi ya African Stars Twanga Pepeta, Asha Baraka akichangia jambo wakati wa
semina fupi ya viongozi na wamiliki wa Bendi za jijini Dar es Salaam.
Meneja
wa Bendi ya Mapacha Watatu, Khamis Dakota akizungumzia tatizo la wanenguaji
kushusha nguo zao mara wanapopandwa na mizuka jukwaani. Alishauri vikundi
visivyosajiliwa vifuatiliwe.
Meneja
wa Ukumbi wa maonesho wa Continental wa jijini Dar es Salaam akielezea maonyesho
yanayofanyika Ukumbini kwake.
Na
Mwandishi Wetu
Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema wiki hii limeendesha semina kwa viongozi na
wamiliki wa bendi nchini ili kusisitiza maadili na utambulisho wa Taifa miongoni
mwa bendi hizo.
Akizungumza
kwenye semina hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa BASATA ulioko Ilala Sharif
Shamba, Katibu Mtendaji wa baraza hilo Ghonche Materego alisema kuwa, ni lazima
sasa wasanii wawe kweli kioo cha jamii, wawe vielelezo na wabebe utambulisho wa
mtanzania.
“Ni
lazima bendi na wasanii wetu kwa ujumla wajiulize hivi kweli wao ni kioo cha
jamii? Wanatoa kweli utambulisho wa mtanzania? Ni vielelezo vya mtanzania?
Tukijiuliza maswali haya tutaweza kujua nini tunafanya katika kulinda utamaduni
wetu” alisema Materego.
Aliongeza
kuwa, wasanii hawana budi kujua jinsi ya kuitumia Sanaa kulingana na hadhira pia
wakati lakini zaidi waweze kuhakiki kazi zao za Sanaa kabla ya kuzipeleka kwa
walaji.
Akinukuu
baadhi ya vipengele kutoka kwenye sera ya Taifa ya Utamaduni, Bw. Materego
alisema kuwa, BASATA kama moja ya mtekelezaji wa sera hiyo ya utamaduni
litahakikisha shughuli zote za burudani nchini hazipotoshi maadili ya
taifa.
“Sera
ya Utamaduni katika sura ya 9 inaeleza haja ya kuchukua hatua kali dhidi ya
wasanii na vikundi vya sanaa vinavyokiuka maadili ya taifa. Tumeona tuwaite
tukumbushane haya kabla hatujafikia hatua hii” alisisitiza
Materego.
Aliongeza
kuwa, Sanaa ni kazi na Baraza lisingependa kukatisha ajira za Wasanii lakini
akasisitiza kuwa, hatua iliyofikia sasa kunahitaji mabadiliko vinginevyo hatua
zitachukuliwa ili kudhibiti udhalili kwenye sekta ya Sanaa.
Kwa
upande wake wamiliki na viongozi wa Bendi walisema kuwa, kumekuwa na tatizo la
wanenguaji wenyewe kushusha nguo zao wanapokuwa kwenye maonyesho lakini
wakaahidi kudhibiti hali hiyo.
“Ni
kweli kuna tatizo hilo la uvaaji hovyo kwenye maonyesho lakini nashauri Baraza
liwe na mfano wa mavazi yatakayotumiwa na wanenguaji lakini pia lifuatilie
vikundi ambavyo havijasailiwa na vinafanya maonyesho yanayovuruga maadili ya
taifa” alishauri Asha Baraka ambaye ni Mkurugenzi wa Bendi ya African Stars
‘Twanga Pepeta’
Comments
Post a Comment