BASATA KUVIJADILI VIKUNDI VYA UNENGUAJI VINAVYOKIUKA MAADILI



PRESS RELEASE
KUWEPO KWA VIKUNDI VYA WANENGUAJI NA BENDI ZINAZOKIUKA MAADILI YA KITANZANIA
Katika siku za karibuni kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa maadili kupitia maonyesho ya majukwaani na kazi mbalimbali za Sanaa.
Kutokana na hali hii, Baraza la Sanaa la Taifa kupitia programu ya Jukwaa la Sanaa Jumatatu ya Tarehe 26/03/2012 litakuwa na mada maalum ya Unenguaji na Maleba Katika Muziki.
Mada hii itakayowasilishwa na Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA) na asasi ya Sanaa ya Binti Leo pamoja na mambo mengine itaangalia hali halisi ya Sanaa ya unenguaji, maleba na matatizo yaliyopo na hatua zinazopaswa kuchukuliwa.
BASATA inatoa wito kwa wadau wote wa Sanaa na wapenzi wa Utamaduni wan nchi yetu kujitokeza kwa wingi siku hiyo kushiriki kuchangia mwelekeo mpya wenye maadili sahihi ya kitanzania.
Sanaa ni Kazi Kwa Pamoja Tuikuze na Kuithamini.
Ghonche Materego
KATIBU MTENDAJI, BASATA

Comments

  1. Tunaimani kuwa Basata itafanya juhudi kuvifuta vikundi vinavyolenga kupotosha maadili ya mtanzania, sijambo jema kuona kila kukicha vinazaliwa vikundi kama vila Kanga Moko na vitu kama hivyo, mbaya zaidi tunatangaziwa hata kwenye vyombo vya habari kuhamasisha watu kwenda kuona huo uchafu, tunatarajia kuona mabaziriko katika kurudisha maadili yetu

    ReplyDelete

Post a Comment