BARCELONA YANG'ANG'ANIWA SAN SIRO


Hivi ndivyo ilivyokuwa, Messi chini ya ulinzi mkali wa Nesta hapa

MABINGWA wa Italia, AC Milan wamewaweka katika wakati mgumu mabingwa wa Hispania, Ulaya na Dunia, Barcelona baada ya kuwalazimisha sare ya bila kufungana usiku huu kwenye Uwanja wa San Siro katika Robo Fainali ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Barca watakuwa katika mgumu kwenye mchezo wa marudiano Uwanja wa Camp Nou, kwa sababu hawakufanikiwa kupata bao ugenini.
Wakati Barca wakitoka uwanjani vichwa chini Milan, Bayern Munich ilinusa Nusu Fainali kwa ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya Marseille, mabao ya Mario Gomez na Arjen Robben.
Barcelona ilitawala mchezo kwa asilimia 62, lakini ilishindwa kupata bao katika mechi ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza ndani ya miaka miwili na nusu.
Kila timu hiyo ya Hispania ilipokuwa ikitengeneza mipango, ilikuwa ikitibuliwa na safu ya walinzi wazoefu ya Milan iliyokuwa ikiundwa na watu kama kipa Christian Abiatti na Jonas Eriksson.
Nafasi pekee ya Lionel Messi kufunga ilikuwa kipindi cha kwanza na pamoja na kutupia mpira nyavuni, lakini bao lilikataliwa kwa sababu aliotea dhahiri kabisa.

Comments