BARCA YAUA 7-1, MESSI TANO PEKE YAKE


MWANASOKA bora wa dunia, Lionel Messi amezidi kudhihirisha ubora wake katika kizazi cha sasa cha soka, kwa kuwekia rekodi nyingine kwa Barcelona kwenye Ligi ya Mabingwa usiku wa jana, wakati APOEL ilipofanya maajabu makubwa kwa kuitoa Lyon kwa penalti.
Messi ameibuka mchezaji wa kwanza kufunga mabao matano katika Ligi ya Mabingwa wakati Barcelona ikiitandika Leverkusen mabao 7-1 kwenye Uwanja wa Camp Noun a kutengeneza ushindi wa jumla mabao 10-2 katika hatua ya 16 bora na kutoa onyo kwa wapinzani wao mbele ya safari.
“Ni mchezaji bora katika historia ya soka ya dunia na hatujawahi kumuona mwingine kama yeye,” alisema kiungo wa Barcelona, Cesc Fabregas kuhusu Messi.
Wakati huo huo APOEL, imesonga mbele kimaajabu kweli kweli, ikiitandika Lyon ya Ufaransa mabao 4-3 kwa penalti baada ya ushindi wao wa 1-0 jana kufanya sare ya jumla ya 1-1.
Kipa wa APOEL iliyow3ahi kumtaka Joseph Kanikio akiwa Simba mwaka 2004, Dionisios Chiotis aliokoa penalti mbili za Lyon na kuiwezesha timu hiyo kung’ara.
Messi alikuwa hashikiki, alifunga mabao mawili kipindi cha kwanzana matatu kipindi cha pili na kufikisha mabao 49 kwenye mashindano yote— hivyo kuungana na Alfredo di Stefano katika nafasi ya nne kwenye orodha ya wafungaji bora wa kihistoria ya Kombe hilo la Ulaya.
Akiwa amefikisha mabao 12 msimu huu, mshambuliaji huyo wa Kiargentina amefikia rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa  Manchester United na Real Madrid, Ruud van Nistelrooy.

Comments