UCHAGUZI MKUU RT SASA APRILI 29



 BAADA ya kuahirioshwa mara kwa mara kwa uchaguzi mkuu wa  Chama cha Riadha Tanzania (RT),  hatimaye kamati ya Utendaji ya RT sasa imepanga uchaguzi huo ufanyike Aprili 29 mwaka huu mkoani Morogoro.
 Katibu Mkuu wa RT, Mujaya Suleimani Nyambui, amesema awali walipanga, katika kikao hicho wangekutana na Kamati ya Uchaguzi ili kupanga tarehe ya usaili, lakini wameamua kuteua kamati ya watu wanne, ambao wataenda kukutana na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Taifa (BMT), Dionis Malinzi ili kujadili jinsi ya kuzipata fedha ambazo zitawasaidia ili kufanikisha uchaguzi huo.

Comments