AZAM YAIPIGA YANGA, YAISHUSHA SIMBA KILELENI


John Bocco kulia akishangilia bao lake la kwanza na said Mourad kushiotoAdd caption

AZAM imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kutimiza pointi 41, kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Yanga iliyokuwa na wahezaji tisa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii.
Mabao ya Azam ambayo hata hivyo imecheza mechi mbili zaidi dhidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili kwa pointi zake 40 na Yanga ya tatu yenye pointi 40 pia, yalitiwa nyavuni na kinara wa mabao Ligi Kuu John Raphael Bocco ‘Adebayor’ dakika ya nne na 82 na lingine Kipre Balou kutoka Ivory Coast dakika ya 55.
Bao la kufutia machozi la Yanga lilifungwa na Mwanasoka Bora wa Uganda, Hamisi Kiiza dakika ya 32.
Katika mechi hiyo iliyotawalia na ubabe baina ya wachezaji wa timu hiyo, Yanga ilipatra hasara ya kupoteza wachezaji wawili, beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ dakika ya 16 tu na kiungo wa Rwanda, Haruna Niyonzima dakika ya 13.
Cannavaro alipewa kadi nyekundu ya moja kwa moja na Niyonzima alipewa kadi ya pili za njano.
Katika mchezo huo, kikosi cha Yanga kilikuwa; Shaaban Kado, Shadrack Nsajigwa, Stefano Mwasyika, Athumani Iddi ‘Chuji’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Nurdin Bakari, Omega Seme, Haruna Niyonzima, Hamisi Kiiza na Shamte Ally.
Azam: Mwadin Ally, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Aggrey Morris, Said Mourad, Bolou Kipre, Tchetche Kipre, Ibrahim Mwaipopo, John Bocco, Salum Abubakar na Mrisho Ngassa.

Comments