AZAM FC:'TUNAIHESHIMU YANGA, LAKINI KICHAPO KAMA KAWA KESHO


WAKATI kesho inashuka katika dimba la Taifa jijini DAr es Salaam kuikabili Yanga, Timu ya soka ya Azam Fc wameapa kuendeleza ubabe wao kwa Wanajangwania hao.
Msemaji wa Azam Fc  Jaffer Iddi Maganga,amesema timu yao ipo tayari kukabiliana na timu yoyote na wakati wote kwani wamefanya maandalizi mazuri ambayo yatawafanya washinde mechi zao zilizosalia na hivyo kuzoa pointi tatu kwqa kila mechi.
Alisema wanaiheshimu Yanga kama timu kongwe lakini kwa suala la uwanjani ni lazima kuwaonyesha makali yao kwani Azam inahitaji pointi zaidi ili kujiimarisha katika nafasi za juu za ligi hiyo.

“Kikosi chetu kipo vizuri na tutaendeleza harakati zetu za kuifunga Yanga kama ilivyokuwa mwaka jana (2011) na hata katika kombe la Mapinduzi mwaka huu na mechi za kirafiki,”Alisema Jaffer.

Comments