AZAM FC WAITIMUA YANGA CHAMAZI

OFISA habari wa Yanga, louis Sendeu akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mechi yao ya kesho dhidi ya Villa Squad kuhamishiwa Uwanja wa Taifa

WAKATI mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga kesho wanakwaana na Villa Squad katika mchezo wa ligi hiyo, Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limehamisha mchezo huo kutoka dimba la Chamazi hadi Uwanja wa Taifa, imefahamika.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Ofisa habari wa Yanga Louis Sendeu alisema kuwa mabadiliko hayo yanafuatia wamiliki wa Uwanja wa Chamazi,Azam Fc kuandika barua TFF kuomba mechi hiyo isipigwe katika dimba hilo kwa hofu ya kutokea vurugu.
“Ndiyo hivyo Villa kama wenyeji wetu huwa wanatumia uwanja wa Chamazi lakini mmiliki wake (Azam FC) ameandika barua TFF kuomba mechi yetru isipigwe huko kwa madai kuwa wanahofia kutokea vurugu kutoka kwa mashabiki wetu,”Alisema Sendeu.
Azam Fc wamelazimika kugomea uwanja wao wakihofia Yanga kuendeleza vuruga walizozifanya mmwishoni mwa wiki iliyopita walipokwaana katika dimba la Taifa na Azam kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.
 Vurugu zilizotokea katika mchezo huo ambao baadhi ya wachezaji wa Yanga walimpiga mwamuzi Israe Nkongo na hivyo kufungiwa kucheza soka kwa nyakati tofauti sambamba na kutozwa faini.

Comments