ARSENAL NOMA, YAKOSA BAO MOJA TU KUISIMAMISHA AC MILAN

KLABU ya AC Milan imenusurika na kusonga mbele katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa matokeo ya jumla ya ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Arsenal , kufuatia jana usiku kufungw3-0 na klabu hiyo ya London.
Ushindi wa Milan 4-0 kwenye Uwanja wa San Siro unazima ndoto za Arsenal kusonga mbele licha ya kushindsa 3-0.
Mabingwa wa Serie A waliduwazwa kipindi cha kwanza na mabao ya Laurent Koscielny, Tomas Rosicky na Robin van Persie aliyefunga kwa penalti.
Milan, ambao wametwaa taji hilo mara saba, walizinduka kipindi cha pili na kuwabana wenyeji hadi kuvuna tiketi hiyo ya kuvuka hatua hiyo ya 16 bora, lakini mashabiki wake walikuwa wana hofu ya kufa katika hatua kama hii kwenye mechi ya marudiano na Deportivo Coruna mwaka 2004.
Katika mchezo huo, Van Persie alipoteza nafasi ya wazi mno ya kufunga bao la kufanya matokeo yawe 4-4.

Comments