ZAMALEK WAIGOMEA YANGA


Na Dina Ismail
UBALOZI wa Misri nchini umegomea maandalizi yote yanayoafanywa na klabu ya Yanga dhidi ya klabu ya soka ya Zamalek ya huko ambayo inatarajiwa kutua nchini alfajir ya Julai 17 kwa ajili ya kukwaana na Yanga katika mechi ya kwanza ya raundi ya awali ya ligi ya mabingwa Afrika itakayopigwa Machi 18 kwenye Uwanja wa Taifa.

Habari za uhakika toka ndani ya ubalozi huo zinaeleza kwamba, baadhi ya maofisa wake wamekuwa wakifuatilia taratibu zote zinazoihusu timu hiyo na kisha kuwasilisha tu mipango kwa klabu ya Yanga.

Imeelezwa kuwa awali Yanga iliwakodia hoteli ya Delux iliyopo maeneo ya Mnazi mmoja lakini maofisa wa ubalozi huo walidai kutoridhishwa na hivyo kwenda kuchukua nafasi katika hoteli ya Golden Tulip, iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam, kabla ya baadaye kuamua kufikia Hyatt Kilimanjaro Kempisk.

“Kweli Yanga iliufanyia oda msafara wa Zamalek ili ufikie katika hoteli ya Delux lakini tumeona hapaendani na hadhi ya klabu yetu hivyo tukaomba kiasi cha fedha waliochopanga kutulipia hapo na sisi tukaongeza chetu,”Alisema ofisa huyo.

Kama hiyo haitoshi, ubalozi pia pia unashughulikia usafiri wa ndani utakaowabeba viongozi, wachezaji na wahusika wengine wa timu hiyo ambao wataambatana nchini na timu hiyo inayotarajiwa kuondoka usiku wa Februari 20,2012.

Katika hatua nyingine Yanga ambayo ipo kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo imepania kushinda mchezo huo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele.

Hata hivyo Zamalek ambayo ilipata kuwa mabingwa wa soka katika bara la Afrika katika miaka ya nyuma itakuja na tahadhari kubwa sana kufuatia kumbukumbu ya kuvuliwa ubingwa wa michuano hiyo na mahasimu wa Yanga, Simba mwaka 2003.

Aidha, timu hizo zote zitashuka dimbani huku zikiandamwa na jinamizi la ukata ambao huenda likachangia kwa namna moja ama nyingine kuwepo kwa matokeo yasiyo ya kuridhisha.

Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHFebruary 18, 2012 at 5:39 AM

    JAMAA WATAONDOKA USIKU WA FEB 20 JE KUNA MIPANGO YEYOTE KWA TIMU ZETU KAMA AZAM AU TIMU ZETU ZA VIJANA NA HATA TAIFA KUPATA FRIEND MATCH HAPO?

    ZAMANI NAKUMBUKA HIZI TIMU ZIKIJA KUCHEZA JUMAMOSI MECHI YA MASHINDANO BASI J2 LAZIMA ITACHEZA MCHEZO WA KIRAFIKI NA AMA YANGA AU SIMBA,SIKU HIZI SISIKII HAYO MAMBO,KULIKONI?

    ReplyDelete

Post a Comment