ZAMALEK KUTUA BONGO ALFAJIR YA FEB 17

WAPINZANI wa Yanga katika klabu bingwa Afrika Zamalek ya Misri inatarajiwa kutua nchini alfajir ya Februari 17 tayari kwa mechi yao dhidi ya Yanga, mchezo utakaopigwa Februari 18 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Ubalozi wa Misri umethibitisha kuwa timu hiyo itakuja siku hiyo kama walivyopanga awali na kufikia katika hoteli ya Golden Tulip kabla ya kuondoka Februari 20.
Ujio wa Zamalek utaondoa utata ulioutawala vichwani vya mwa washabiki wa soka nchini ambao walitaraji wasingewasili kufuatia machafuko yaliyotokea nchini mwao hivi karibuni  baada ya baada ya Al-Ahly kushinda mabao 3-1 na mashabiki kuvamia Uwanja kuwakimbiza wachezaji na ndipo yakaanza mapambano baina mashabiki wa pande hizo mbili na kusababisha watu 74 kuuawa na wengine 1,600 kujeruhiwa.
Kutokana na hali ligi Kuu ya Misri ilisimamishwa kabla ya  baadaye Waziri Mkuu wa Misri, Kamal el-Ganzouri kuwafukuza viongozi wote wa Shirikisho la Soka la Misri (EFA) na kuagiza wahojiwe na polisi kuhusiana na  vurugu hizo.

Comments