YANGA YARUHUSU NYOTA WAKE KUIVAA MAMBAS

SHABAN KADO

UTATA kuhusu wachezaji wa Yanga waliopo timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kucheza mechi ya mchujo ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Msumbiji, umemalizika baada ya kikosi cha Yanga kutarajiwa kuondoka nchini Machi Mosi kwenda Cairo, Misri tayari kwa mechi yao ya marudiano ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Zamalek ya huko.
Awali uongozi wa Yanga ulipinga wachezaji wake waliopo Stars, Shaban Kado, Stephen Mwasika na Shadrack Nsajigwa kucheza mchezo huo kwa madai ya kuhofia kupata muda wa kuungana nao katika safari ya nchini Misri tayari kwa mechi hiyo itakayopigwa Machi 4.
Habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana kutoka ndani ya klabu ya Yanga zinasema kuwa nyota Shaban Kado, Shadrack Nsajigwa na Stephano Mwasyika wameruhusiwa kucheza mechi hiyo kutokana na ukweli kwamba hakuta kuwa na safari ya mapema kama ilivyodaiwa awali baada ya kuwepo kwa utata juu ya mechi hiyo.
Mmoja ya viongozi wa Yanga alisema kwamba kutokana na kuwa na muda wa kutosha kabla ya safari hiyo hawana umuhimu wowote wa kuwahi Misri hivyo hawana sababu ya kutowaruhusu wachezaji wao ili kuitumikia timu ya Taifa.
Katika mchezo wa awali ulipogwa jumamosi iliyopita katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

Comments