YANGA YAKARIBIA KITI VPL


MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga, wamechumpa hadi nafasi ya kwanza katika ligi hiyo baada ya kuibanjua Mtibwa Sugar ya Morogoro kwa mabao 3-1,kupitia mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa TAifa.
MAtokeo hayo yanaifanya Yanga kufikisha pointi 34 kupitia mechi 16 ilizocheza kwenye ligi hiyo huku mahasimu wao wa jadi, Simba wakiendelea kukalia kilele hicho licha ya kuwa sawa na Yanga kwani Simba nayo ina pointi 34 baada ya kucheza mechi 16.
Hata hivyo Yanga ina mabao ya kufunga 28 ya kufungwa 13 huku Simba ikiwa na mabao 25 ya kufunga, na 10 ya kufungwa hivyo kuwa sare sare.

Comments