YANGA SC HAOOO MILINGOTINI

MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga, keshokutwa wataingia kambini Wilaya ya  Bagamoyo, Pwani ikiwa ni mahususi na kujiandaa na mchezo wao wa awali wa ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zamalek ya Misri, imefahamika.
Timu hizo zinatarajiwa kukwaana Februari 18 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo wapinzania wao hao wanatarajiwa kuwasili Februari 17.
 Mmoja ya viongozi wa Yanga amesema kwamba timu itaingia kambini mara baada ya kumalizika kwa mechi ya ligi kuu baina ya timu hiyo na African Lyon.
Alisema  kuwa wanaamini kambi hiyo ya nje ya mji itawaweka vizuri zaidi kutokana na kuwa wachezaji watakuwa kwenye hali ya utulivu ya kujiandaa na mchezo huo.
“Naamini kambi hiyo ya wiki moja itaiweka vizuri zaidi timu yetu katika kujiandaa na mchezo wetu na Zamalek ambao naaamini utakuwa na upinzani mkubwa,”Alisema Kiongozi huyo.
Yanga inayonolewa na Mserbia Costadin Papic, imekuwa ikitumia zaidi michezo ya ligi kuu kujiandaa na mechi hiyo, huku wapinzani wao wakijifua kwa siri sambamba na kuzuia mashabiki kuhudhuria uwanjani.

Comments