YANGA, RUVU WAINGIZA MILIONI 47


WATU 14,150 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Ruvu Shooting lililochezwa jana (Februari 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuingiza sh. 47,554,000. Hata hivyo ni watazamaji saba tu waliokata tiketi za VIP A zilizokuwa zikiuzwa sh. 15,000. Viingilio vingine vilikuwa sh. 10,000 kwa VIP B na C, sh. 5,000 viti vya rangi ya chungwa na kiiingilio cha sh. 3,000 kwa viti vya bluu na kijani kilichovutia watazamaji 12,853. Baada ya kuondoa gharama za awali za mechi hiyo namba 119 na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 7,254,000 kila timu ilipata sh. 8,583,000 wakati mgawo wa uwanja ulikuwa sh. 2,861,000. Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,144,400, TFF sh. 2,861,000, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,430,500, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 286,100 na asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 2,861,000. Gharama za awali za mechi ni nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna sh. 10,000, posho ya kujikimu kamishna sh. 40,000, posho ya kujikimu waamuzi sh. 120,000 na mwamuzi wa akiba sh. 30,000. Gharama za tiketi sh. 4,000,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000. Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata sh. 990,500 wakati DRFA ilipata sh. 849,000.

Comments