Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha soka (FAT) sasa
(TFF), Michael Wambura amewasilisha rasmi barua ya pingamizi dhidi ya
mgombea wa Uenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Amin
Bakhressa.
Wambura amesema amewasilisha barua yake DRFA na kupokelewa na mjumbe wa
Kamati ya Uchaguzi Kanuti Daudi alisema kwamba Katiba ya DRFA ibara ya 29 (3)
inamtaka mgombea kuwa na sifa zilizoainishwa kwenye ibara ya 30(2) ya elimu ya
kidato cha nne, huku ibara ya 9 ya kanuni za uchaguzi wa wanachama wa TFF
inamtaka mgombea yeyoye lazima awe na elimu ya kidato cha nne inayoambatana na
cheti cha matokeo.
“Kwa
mantikiti hiyo Amin Mohammed Salim (Bakhressa) anakosa sifa ya kuwa mgombea
Uenyekiti wa DRFA kwa kuwa hana elimu ya kidato cha nne kinachoambatana na
cheti cha matokeo, hivyo jina lake liondolewe katika orodha ya wagombea
waliopitishwa kugombea uongozi wa DRFA,”Alisema Wambura.
Aidha,
Wambura pia amewatolea pingamizi wapiga kura wa DRFA Abeid Mziba (Kinondoni),
Saleh Ndonga (Temeke) na Amar Balhaboo (Ilala)
ambao nao wanadaiwa kutokuwa na elimu ya kidato chga nne pamoja cheti
cha matokeo.
“Naomba kamati
itamke wazi kuwa viongozi hao walichaguliwa kimakosa bila kuzingatia kanuni za
uchaguzi za TFF hivyo nafasi zao zitangazwe ziko wazi ili wapatikane watu wenye sifa za kikanuni
kugombea,”Aliongeza Wambura.
Uchanguzi
wa DRFA umepangwa kufanyika Machi 18 katika sehemu ambayo itatangazwa ambapo
kamatyi ya uchaguzi chini ya mwenyekiti wake Alhaj Muhidin Ndolanga imeshafanya
usaili na kutanga majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali.
MICHAEL BWANA HAISHI VITUKO,HIVI ANADHANI ATAMUWEZA HUYO AMIN?HUYO NDIO BINGWA WA TANZANIA FOOTBALL FITNA-TFF,MICHAEL MWENYEWE KAPITIA MIKONONI KWAKE NDIO AKAFANIKIWA KUINGIA KWENYE MPIRA,HALAFU PIA MICHAEL AKUMBUKE KWAMBA MWENYEKITI WA UCHAGUZI NI ALHAJJ!POA TUSUBIRI TUONE HUO MPAMBANO WA MWALIMU NA DENTI
ReplyDeleteOTHERWISE MAMA SIMBA NAONA UMEKUJA KIVINGINE NA BLOG YAKO,HII RANGI YA BACKGROUND NI NZURI LAKINI MIMI MWENZENU SIJUI KWANINI SIIPENDAGI,NAONA NINA ALLERGY NAYO DIZAINI
SAYZ MDAU WA BOMBA,REVERE,MASACHUSSETTS,US