WAALIKWA TU KUHUDHURIA MAZISHI WHITNEY HOUSTON JUMAMOSI


MAZISHI ya gwiji  la muziki nchini Marekani  Whitney Houston  yanatarajiwa kufanyika jumamosi katika kanisa ambalo alianza enzi za utoto wake.
Taarifa zinaeleza kwamba wahudhuriaji wa mazishi hao ni wale watakaopewa nialiko maalum huku,  kampuni iliyopewa kuendesha shughuli za mazishi hayo hakutakuwa na zoezi la wazi kwa ajili ya kuaga mwili wa marehemu
Houston (48) alifariki jumamosi iliyopita katika hoteli huko  Beverly Hills, California,saa chache kabla ya kupanda jukwaa kutumbuiza katika hafla ya matayarisho ya tuzo za Grammy ambapo mwili wake ulikutwa ukielea kwenye maji katika bafu la chumba cha hoteli alilopangwa.




Comments