KOCHA wa
Simba, Cirkovic Milovan na mshambuliaji Emmanuel Okwi walijikuta kwenye wakati
mgumu mbele ya maafisa uhamiaji wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere juzi.
Maafisa
uhamiaji hao waliwazuia Milovan na Okwi kwa zaidi ya dakika kumi kutokana na
vibali vyao vya kufanya kazi nchini kuwa vya muda mfupi na pia siku zake za
kumalizika zinakaribia.Kutokana na hali hiyo, viongozi wa Simba wakiongozwa na
Katibu Evordus Mtawala waliingia kati na kuomba waruhusiwe kwani suala hilo
linashughulikiwa kwa haraka.
Akizungumza
na gazeti hili baada ya kuruhusiwa, Milovan alisema kibali changu kimebakiza
siku 15 na viongozi wanajua, lakini wanashindwa kulitatua."Kila siku na
namueleza Mtawala suala hili, lakini yeye atakwambia kesho hadi sasa hajafanya
hivyo si kitu kizuri kusumbuliwa hivi."
"Nashindwa
kufanya kazi vizuri, kutokana na usumbufu wa aina hii, nataka viongozi kesho
(leo) waanze kufutilia jambo hili," alisema Milovan ambaye suala kibali
chake pia lilikuwa tatizo kwenye uwanja wa ndege wa Kigali , Rwanda .
Naye makamu
mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange Kaburu alisema ni kweli kibali cha kocha na
wachezaji wao wa kigeni vilikuwa vimekatwa vya muda mfupi."Vibali vyao
wote vimebakiza siku 15, lakini ni suala tutakalolishughulikia kwa haraka ili
kuondoa usumbufu huu," alisema Kaburu.
Naye katibu
Mtawala alisema ni kweli kocha amekuwa akimkumbusha kila wakati kuhusu suala
hilo.
"Unajua
kuna watu watano ambao tunapaswa kulipia vibali vyao na kibali kimoja dola
2000, watano dola 10,000 si fedha ndogo.
"Tutalimaliza
suala hili wiki hii kwa sababu siku 15 si nyingi tunaweza kupata usumbufu
mwingine na watu wa uhamiaji," alisema Mtawala.
Katika
wachezaji watatu na makocha wawili waliosafiri na Simba kwenda Rwanda ni
kiungo Partick Mafisango pekee aliyekuwa na kibali cha muda mrefu cha kufanya
kazi nchini alichokatiwa na klabu ya Azam.
Comments
Post a Comment