TWANGA PEPETA KUVALENTINE TEMEKE

Bendi ya African Stars maarufu kama Twanga Pepeta, itatambulisha nyimbo zao mpya kwenye onyesho lao la Valentine litakalofanyika Februari 14 kwenye ukumbi wa Equator Grill, Temeke.

Onyesho hilo limeandaliwa na Keen Arts na Bob Entertainment chini ya udhamini wa Dodoma Wine na Freditto Entertainment.

Mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka, alisema jana kuwa siku hiyo ya Februari 14 ambayo huadhimishwa na wapendanao duniani kote, watatumia kutambulisha nyimbo zao mpya ambazo zitakuwepo kwenye albamu mpya inayofuata “Dunia Daraja”.

Asha aliwaomba wapenzi wa muziki wajitokeze kwa wingi siku hiyo ili wasikilize tungo zao mpya na rapu mpya,” alisema Asha.

Bendi hiyo inaundwa na wanamuziki machachari kama akina Dogo Rama, Msafiri Diouf, Amigolas, Haji, Vena, Saleh Kupaza, Luiza Mbutu, Khadiji Mnoga na Janet Isinika na Muumin Mwinjuma katika safu ya uimbaji.

Katika safu ya upigaji vyombo wapo

Jojo Jumanne, Thabiti Abdul, Miraji Shakashia, Gody Kanuti, Kado, Victor Mkambi, James Kibosho, MCD na wengineo.

Comments