Alex
Mgongolwa,Mwenyekiti Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Februari
21, 2012
Kamati ya
Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
ilikutana Februari 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam na kufanya uamuzi kwa
ajenda mbalimbali ikiwemo Marekebisho ya Katiba za Wanachama wa TFF, na pia
ushauri wa kisheria ulioombwa kwake na Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
Uamuzi
uliofanywa kwa wanachama wote 40 wa TFF ni ufuatao; wanachama wote wanatakiwa
kufanya marekebisho kwenye katiba zao katika maeneo matatu kwa mujibu wa
maelekezo ambayo TFF ilitoa mwaka jana.
Maeneo hayo
ni sifa za wagombea uongozi ambapo kwenye kipengele cha elimu ni lazima iwe
kuanzia kidato cha nne, kutopeleka masuala ya mpira wa miguu katika mahakama za
kawaida na kamati zao za uchaguzi kufanya kazi chini ya Kamati ya Uchaguzi ya
TFF.
Hivyo
hakuna mwanachama yeyote wa TFF anayeruhusiwa kufanya uchaguzi kwa sasa kama katiba yake ina upungufu au inakwenda kinyume na
maelekezo kuhusu maeneo hayo matatu.
Kamati
imetoa hadi Juni Mosi mwaka huu kwa wanachama ambao katiba zao zina upungufu
katika maeneo hayo wawe wamefanya marekebisho ndiyo waendelee na uchaguzi kwa
wale ambao muda wa uchaguzi umefika.
Ushauri wa
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji kwa Kamati ya Uchaguzi ya TFF
ni kuwa katiba zote za wanachama ziwe na vitu hivyo vitatu.
Alex
Mgongolwa
Mwenyekiti
Kamati ya
Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji
Comments
Post a Comment