STEVE WONDER, ARETHA FLANKLIN KUTUMBUIZA MAZISHI YA WHITNEY HOUSTON

NEW JERSEY, Marekani


WAIMBAJI Aretha Franklin na Stevie Wonder wanatarajiwa kuimba kwenye maziko ya mwimbaji, Whitney Houston anayetarajiwa kuzikwa kesho jirani na kanisa alilokuwa akiimbia utotoni New Hope Baptist la Newark.
Mwimbaji Kristen Foster pia amethibitisha kushiriki kuimba katika maziko hayo akiwa amepewa mualiko na mume wa zamani wa Houston, Bobby Brown.

Wengine wataoshiriki ni mwanamuziki nguli, Clive Davis, anatarajiwa kuzungumza katika maziko hayo, mwimbaji wa injili na rafiki mkubwa wa familia Marvin Winans.

Wengine wanaotarajiwa kushiriki katika maziko hayo ni Donnie McClurkin, Tyler Perry, Kim Burrell, Rickey Minor, Alicia Keys, Dionne Warwick na Cece Winans, Foster na wengineo.

Houston alifariki jumamosi jijini Beverly Hills, California akiwa na umri wa miaka 48.

Comments