SIMBA YAPANIA KUYEYUSHA KONI ZA AZAM KESHO

KOCHA mkuu wa timu ya soka ya Simba MIlovan Cirkovic ameapa kuiadhiri Azam Fc kupitia mchezo wao wa ligi kuu soka Tanzania Bara utakaopigwa kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na mechi yao hiyo alisema kuwa anafahamu umahiri walionao vijana wa Azam lakini hiyo si sababu ya vijana wake kushindwa kuwafunga.
"Nafahamu ubora iliyonayo Azam Fc lakini hilo si jibu kuwa watatufunga...nimekindaa vema kikosi changu na nina uhakika ushindi utapatikana,"Alisema Milovan.
Aidha Mserbia huyo aliongeza kuwa katika mchezo huo huenda nyota Felix Sunzu akashuka dimbani kwani kwa sasa hali yake imeimarika.
Hata hivyo, Milovan alisema kuwa wachezaji wake wote wapo katika hali nzuri isipokuwa beki wake Amir Maftah na kiungo Jonas Mkude ambao ni majeruhi.

Comments