SIMBA, YANGA ZATIMULIWA CAF


Klabu za Zamalek ya Misri na Kiyovu Sport zimekataa maombi ya mechi zao za marudiano za Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga na Simba kusogezwa mbele kwa wiki moja kutoka wikiendi ya Machi 2, 3 na 4 mwaka huu.
Baada ya mazungumzo na klabu za Simba na Yanga, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilituma maombi Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuomba mechi hizo zisogezwe ili wachezaji wapate fursa ya kutosha kuzitumikia klabu zao na timu ya Taifa (Taifa Stars).
Februari 29 mwaka huu Taifa Stars itacheza mechi ya mchujo ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa ajili ya fainali za mwakani nchini Afrika Kusini dhidi ya Msumbiji kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wikiendi ya Machi 2, 3 na 4 mwaka huu Yanga itakuwa inarudiana na Zamalek ugenini wakati Simba itarudiana na Kiyovu Sport jijini Dar es Salaam. CAF ilikuwa tayari kuridhia maombi hayo iwapo Chama cha Mpira wa Miguu cha Misri (EFA) na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Rwanda (FERWAFA) wangekubali.
Lakini EFA na FERWAFA wamekataa ombi hilo kwa vile litavuruga ratiba ya mechi za ligi katika nchi hizo.

Comments