SIMBA WAIPANIA KIYOVU KESHO


WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho  Simba wameapa kufia uwanjani kesho katika dimba la Journal mjini Kigali, Rwanda ambapo watakwaana na Kiyovu ya huko. 
Simba iliwasili jana mjini humo na kufikia  katika Hotel ya Sports View ambapo jioni ya leo itafanya mazoezi katika dimba la Amahoro.
Wachezaji wa Simba chini ya kocha wao Mserbia Milovan Cirkovic pamoja na kusema mechi hiyo itakuwa na ushindani mkubwa, watatuamia vema mafunzo waliyopewa na kocha wao kuhakikisha wanaibuka na ushindi.
Kikosi cha Simba kilichopo huko kinaundwa na  makipa Juma Kaseja, Ally Mustafa 'Barthez' mabeki ni  Juma Jabu, Said Nassor 'Cholo', Obadia Mungusa, Victor Costa, Juma Nyoso, Kelvin Yondani, wakati  viungo ni Shomari Kapombe, Mwinyi Kazimoto, Patrick Mafisango, Jonas Mkude, Salum Machaku, Uhuru Selemani na Edward Christopher  huku  washambuliaji ni Felex Sunzu, Emmanuel Okwi na Ramadhan Singano.

Comments