ROONEY AIWEKA KILELENI MAN UNITED


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa England, Wayne Rooney leo amefunga mabao mawili peke yake yaliyoipa Manchester United ushindi wa 2-1 dhidi ya Liverpool kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Ushindi huo unawapandisha kileleni mwa Ligi Kuu ya England Mashetani hao Wekundu, baada ya kufikisha pointi 58 kutokana na mechi 18.
Manchester City wanaweza kurejea kileleni mwa Ligi Kuu iwapo wataifunga Aston Villa leo.
Wachezaji wa timu zote ilibidi watenganishwe jana wakati wamapumziko, baada ya mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez kugoma kupeana mikono na beki wa United, Patrice Evra mwanzoni kwenye mchezo huo.
Suarez alikuwa akicheza kwa mara ya kwanza tangu amalize adhabu yake ya kufungiwa mechi nane kwa kumfanyia kejeli za kibaguzi Evra Oktoba, mwaka jana.
Rooney alifunga mabao yote mawili ndani ya dakika nne za kipindi cha pili, kabla ya Suarez kufunga la kufutia machozi dakika ya 80.

Comments