REAL MADRID YARAHISISHA KAZI ULAYA

MCHEZAJI Pontus Wernbloom alifunga katika dakika ya tatu ya muda wa nyongeza na kuiwezesha timu yake CSKA Moscow kupata sare ya 1-1 na Real Madrid katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu.
Wernbloom alikutana na mpira ambao ulimbabatiza beki wa Madrid, Alvaro Arbeloa na kuusukuma nyavuni.
Katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Luzhniki mjini Moscow, Urusi, Mreno Cristiano Ronaldo aliifungia Real Madrid bao la kuongoza dakika ya 28, hilo likiwa bao lake la 36 msimu huu.
Mechi ya marudiano baina ya timu hizo itapigwa Hispania Machi 14, mwaka huu.

Comments